YOU ARE NOT ALONE

"I can’t give solutions to all of life’s problems, doubts, or fears. But I can listen to you, and together we will search for answers."

MUST WATCH...

Loading...

karibuni

Karibuni katika blog yetu ambayo itakuwa ikizungumzia kuhusu masuala ya uzazi hasa kwa wale wenye matatizo ya kuchelewa kupata watoto (infertility). Hapa tutajadili chanzo cha matatizo hayo na njia zinazoweza kutumika kuondoa tatizo hilo pamoja na kupeana ushauri na nasaha katika masuala mbalimbali yanayohusu uzazi. "KWA NEEMA YA MUNGU KILA MWANAMKE ATANYONYESHA"

Monday, 24 March 2014

Kufuatilia siku za mzunguko wa mwezi

Ni ukweli usiopingika kuwa asilimia kubwa ya wanawake hatujui ama tunashindwa kuzifatilia vizuri siku zetu za mzunguko wa mwezi. Hali hii kwa kiasi kikubwa inachangia kushindwa kupata ujauzito (ukiachilia mbali na matatizo mengineyo), hivyo ni muhimu sana kwetu wasaka kuzijua siku zetu na mzunguko mzima unavyokwenda kuanzia siku ya kwanza unayoingia mwezini hadi mzunguko mwengine wa mwezi unaofuatia. Hii itasaidia sana kukujuulisha ni siku zipi nzuri kwa kusaka ili usiziruke na uongeze bidii. Pia kwa wale wanaotumia dawa kuna dawa unatakiwa kuzitumia kwa siku maalum katika mzunguko mfano siku ya saba (7) au kumi na moja (11) hivyo ukiwa na uelewa wa kutosha na ukizifatilia siku kwa usahihi unaweza kuwa katika nafasi nzuri sana kwa mzunguko husika. 
Kawaida ufatiliaji hufanyika kwa kutumia KALENDA ambayo unarekodi siku ya kwanza ya mzunguko wako na kadiri siku zinavyoendela, njia hii ni ya kizamani (kiasili) na kwa mtu asiekuwa na elimu ya kutosha inaweza kukusumbua zaidi badala ya kukusaidia. 
Kutokana na maendeleo ya kiteknolojia, sasa mambo yamerahisishwa kiasi kwamba mtu yoyote awaweza kurekodi kumbukumbu zake kieletroniki na kupata msaada pale anapokwama, kwa wanaotumia simu za kisasa mambo yamekuwa rahisi zaidi kwani unaweza kuweka rekodi zako muda wowote. 
kwa yeyote anaetumia simu ambayo anaweza kupata play store, apps zifuatanzo ni nzuri sana kuwa nazo kwani zinasaidia kutrack tarehe zako na activities zote muhimu katika usaka. 
Kwa kufatilia ovulation ya kawaida:
  1.  Ovu View - ovulation and fertility
  2. Fertility Friend Mobile

Kwa wanaofanya ivf:
  • My fertility diary (unaweza ukatumia na hizo hapo juu pia)

unaweza kudownload moja wapo au zote kwani haina tatizo lolote, mimi binafsi natumia zote kwani moja ikikosea kidogo nyengine inakuongoza na sio mbaya kuwa na second opinion mwisho wa siku na wewe unaingiza mawazo yako. 
Naombeni tumieni halafu mtuambie maoni yenu ili kuwasaidia na wengine.

Friday, 21 March 2014

TUNARUDI HEWANI

Habari za siku nyingi wapendwa.

Kutokana na sababu mbali mbali za kifamilia na binafsi (ikiwemo shule), nilipumzika kuweka post kwa muda mrefu, hata hivyo ndani ya muda wote huo nimekuwa nikipokea emails mbali mbali kutoka kwa wasaka wenzangu zikiniomba niendelee kublogua. Katika siku tatu zilizopita email zimeongezeka na kuna ambazo zina ujumbe mzito sana kiasi ya kwamba ilinibidi nikae chini na kufikiria maamuzi yangu tena. Nimewaza na kujiuliza:-
- hivi ni lipi lengo la kuanzisha hii blog na sasa niwaache mkono wasaka wenzangu ambao wanahitaji mahali pakusemea shida zao na mahali pa kupumua wakati nayajua fika magumu na maumivu ya tatizo hili hasa unapokua mpweke?

Baada ya kupata majibu ya suali hilo nimeamua kurudi tena hewani kwa lengo lile lile la kusaidia, kupeana ushauri, kufarijiana, kupeana nguvu na moyo ili tuweze kupambana na hili tatizo letu, hivyo basi nawatangazia rasmi kuwa tutaanza kublogua kuanzia  Jumaatatu tarehe 24 March 2014.

Kwa kweli ushirikiano wenu unahitajika sana ili tuweze kufanikiwa na lengo letu litimie. nakaribisha mtu mwenye makala yoyote ambayo inahusiana na usaka, maswali, maoni,  ushauri, ujumbe, ushuhuda hasa kwa waliofanikiwa ili waweze kuhamashisa wengine, n.k. 
Nawashukuru sana kwa umoja na ushirikiano wenu.
Msaka mimi,
Chaby

Note: nakaribisha maoni pia kuhusu muonekano mzima wa blog nini tuongeze na nini tupunguze ili kuipendezesha.