YOU ARE NOT ALONE

"I can’t give solutions to all of life’s problems, doubts, or fears. But I can listen to you, and together we will search for answers."

karibuni

Karibuni katika blog yetu ambayo itakuwa ikizungumzia kuhusu masuala ya uzazi hasa kwa wale wenye matatizo ya kuchelewa kupata watoto (infertility). Hapa tutajadili chanzo cha matatizo hayo na njia zinazoweza kutumika kuondoa tatizo hilo pamoja na kupeana ushauri na nasaha katika masuala mbalimbali yanayohusu uzazi. "KWA NEEMA YA MUNGU KILA MWANAMKE ATANYONYESHA"

Thursday 13 December 2012

Speak out

kuchelewa kupata mtoto ni jambo linaloumiza sana, linaumiza kutokana na mtazamo wa jamii  na wanafamilia juu ya wahusika na pia  hamu ya wanandoa kutamani kupitia hatua muhimu ya maisha (kujenga familia).  Ni ukweli usiopingika kuwa maumivu haya hayana mfano wa kitu chochote duniani, hasa pale muhusika anapokuwa anapambana na unyanyapaa na kulazimika kuikana hali aliyonayo ili jamii imuone kuwa yupo sawa na wengine. 
Mitazamo inatofautiana, lakini mimi binafsi nimeona kujikubali na kukubali kwa watu kuwa nina tatizo, imenisaidia sana kupunguza mzigo wa machungu kifuani mwangu na pia utitiri wa maswali kuwa utazaa lini??, bado tu??  acha uvivu?? SIONI AIBU KWA NILIVYO, NADHANI NA WAKATI UMEFIKA SASA KWA WASAKA WENZANGU KUFUNGUKA.....

No comments:

Post a Comment