Habari za siku nyingi wapendwa.
Kutokana na sababu mbali mbali za kifamilia na binafsi (ikiwemo shule), nilipumzika kuweka post kwa muda mrefu, hata hivyo ndani ya muda wote huo nimekuwa nikipokea emails mbali mbali kutoka kwa wasaka wenzangu zikiniomba niendelee kublogua. Katika siku tatu zilizopita email zimeongezeka na kuna ambazo zina ujumbe mzito sana kiasi ya kwamba ilinibidi nikae chini na kufikiria maamuzi yangu tena. Nimewaza na kujiuliza:-
- hivi ni lipi lengo la kuanzisha hii blog na sasa niwaache mkono wasaka wenzangu ambao wanahitaji mahali pakusemea shida zao na mahali pa kupumua wakati nayajua fika magumu na maumivu ya tatizo hili hasa unapokua mpweke?
Baada ya kupata majibu ya suali hilo nimeamua kurudi tena hewani kwa lengo lile lile la kusaidia, kupeana ushauri, kufarijiana, kupeana nguvu na moyo ili tuweze kupambana na hili tatizo letu, hivyo basi nawatangazia rasmi kuwa tutaanza kublogua kuanzia Jumaatatu tarehe 24 March 2014.
Kwa kweli ushirikiano wenu unahitajika sana ili tuweze kufanikiwa na lengo letu litimie. nakaribisha mtu mwenye makala yoyote ambayo inahusiana na usaka, maswali, maoni, ushauri, ujumbe, ushuhuda hasa kwa waliofanikiwa ili waweze kuhamashisa wengine, n.k.
Nawashukuru sana kwa umoja na ushirikiano wenu.
Msaka mimi,
Chaby
Note: nakaribisha maoni pia kuhusu muonekano mzima wa blog nini tuongeze na nini tupunguze ili kuipendezesha.
Note: nakaribisha maoni pia kuhusu muonekano mzima wa blog nini tuongeze na nini tupunguze ili kuipendezesha.
No comments:
Post a Comment