The world of achievement has always belonged to the optimist.
J. Harold Wilkins
Yes, I will fight... I knock it once and I will do again. My status now is upgraded, from Primary infertile to Secondary Infertile. What a tittle??? Senior Infertile..... Sound good eeeehh!!! hahaha
YOU ARE NOT ALONE
"I can’t give solutions to all of life’s problems, doubts, or fears. But I can listen to you, and together we will search for answers."
karibuni
Karibuni katika blog yetu ambayo itakuwa ikizungumzia kuhusu masuala ya uzazi hasa kwa wale wenye matatizo ya kuchelewa kupata watoto (infertility). Hapa tutajadili chanzo cha matatizo hayo na njia zinazoweza kutumika kuondoa tatizo hilo pamoja na kupeana ushauri na nasaha katika masuala mbalimbali yanayohusu uzazi. "KWA NEEMA YA MUNGU KILA MWANAMKE ATANYONYESHA"
Friday, 23 March 2012
Wednesday, 21 March 2012
Special Dedication; kwa wanawake wote ambao wana matatizo ya uzazi
nimekutana na wimbo huu ambao ni Dedication kwa wanawake wote duniani wanaopambana na majaribu ya kukosa mtoto. Nami nautoa kwa wasaka wenzangu wote ambao wanajitambua, wasiokata tamaa, wanaoendelea kupambana na kujaribu kwa kila ambalo lipo ndani ya uwezo wao. pamoja na jitihada zote na kuwa bado hujafanikiwa usikate tamaa na kujiona hufai, daima kumbuka kuchelewa kwako kupata mtoto hakubadilishi uwanamke wako. ukiwa na imani na tamaa utafanikiwa
Thursday, 15 March 2012
JIACHE: Positive Test result
kwa wale wasaka wenzangu, najua twaisubiri kwa hamu saaaaaaana, itafika very soon, be positive
Hebu jiachie uniambie itakuwaje siku hii?
Hakuna lisilowezekana chini ya jua, na ukipata matitabu sahihi infertiility inatibika.
"kwa neema ya mungu kila mwanamke atanyonyesha."
Tuesday, 13 March 2012
Monday, 5 March 2012
Safari ya Wasaka, Maandalizi yaanza
Msaka mimi pamoja na wenzangu tunaianza safari kwa kutumia ilee siri yetu.
YESS, kwa umoja wetu tunaianza safari hii, ingawa hatujui twendako kutakuwaje lakini tumejawa na matumaini tele, tunaamini mungu atatuonesha njia ili tufike salama soooote kwa pamoja, hakuna kuachwa mtu njiani ikibidi hadi kwa machela tutabebana mradi tufike pamoja.
maandalizi ya safari yetu yameanza, kikosi lazima kiwe na jezi ati! kujua kikosi kinaundwa na nani na mpiganaji yupi anavaa namba ipi... stay tuned. nitakupasha hatua kwa hatua.
hii ndio silaha yetu.
tunahitaji sala na dua zenu
Saturday, 3 March 2012
Mwezi Wetu
Yap ni mwezi wetu, ni JUNE- WORLD INFERTILITY MONTH, ndio hivyo mdau na sisi tunao mwezi wetu, hii ni kukuonesha kuwa haupo peke yako, dunia nzima inakutambua. Mwezi huu una lengo la kutoa elimu na uelewa juu ya kujaribu na mafanikio ya kupata ujauzito. Wataalamu mbali mbali duniani hukutana na kujadili njia zinazoweza kusaidia, huangalia mapungufu yanayojitokeza, changamoto na maazimio mapya huwekwa, hii yote ni katika kukusaidia wewe mdau . mwezi huu unasherehekewa ili watu waelewe, watoe msaada (support), wajifunze na kuchukua hatua katika kufanikiwa kupata watoto.
sasa kama dunia inakutambua kwanini na wewe usijitambue? usikate tamaa, waliofanikiwa hawana miujiza ya ajabu zaidi yako, wote walihangaika kama ulivyo wewe sasa, naomba ninukuu maneno haya
"no matter if it takes you months or years to finally conceive..... or if, sadly, you are unable to do and decide to go a different route, the feelings and emotions you and/or your significant other experience can be indescribable. Infertility is difficult, yet treatable most of the time! There is hope......Don't give up! (Rebecca Waterfield, Roanoke Holidays Examiner)
yess dear, there is hope......don't give up!!
Be positive, you will do it.
Subscribe to:
Posts (Atom)