YOU ARE NOT ALONE

"I can’t give solutions to all of life’s problems, doubts, or fears. But I can listen to you, and together we will search for answers."

karibuni

Karibuni katika blog yetu ambayo itakuwa ikizungumzia kuhusu masuala ya uzazi hasa kwa wale wenye matatizo ya kuchelewa kupata watoto (infertility). Hapa tutajadili chanzo cha matatizo hayo na njia zinazoweza kutumika kuondoa tatizo hilo pamoja na kupeana ushauri na nasaha katika masuala mbalimbali yanayohusu uzazi. "KWA NEEMA YA MUNGU KILA MWANAMKE ATANYONYESHA"

Monday 5 March 2012

Safari ya Wasaka, Maandalizi yaanza

Msaka mimi pamoja na wenzangu tunaianza safari kwa kutumia ilee siri yetu.

YESS, kwa umoja wetu tunaianza safari hii, ingawa hatujui twendako kutakuwaje  lakini tumejawa na matumaini tele, tunaamini mungu atatuonesha njia ili tufike salama soooote kwa pamoja, hakuna kuachwa mtu njiani  ikibidi hadi kwa machela tutabebana mradi tufike pamoja.

maandalizi ya safari yetu yameanza, kikosi lazima kiwe na jezi ati! kujua kikosi kinaundwa na nani na mpiganaji yupi anavaa namba ipi... stay tuned. nitakupasha hatua kwa hatua.


hii ndio silaha yetu.
tunahitaji sala na dua zenu

2 comments:

  1. nashukuru sana kwa kunipa moyo nimejisikia faraja ya ajabu.mie msaka kama wewe..nilishakutumia email na umeshanijibu kuhusu kuijua siri..sasa usitoe namba zetu za simu hadharani huku tutakuwa tunatumia nick names ( a.k.a)..Twende pamoja hakuna kubaki nyuma lazima ninyonyeshe...

    ReplyDelete
  2. sote tunaelewa uzito wa hili jambo, usijali dear sitatoa namba ya simu au utambulisho wa mtu yoyote bila ya ruhusa yake. uko pamoja "kwa neema ya mungu kila mwanamke atanyonyesha"

    ReplyDelete