YOU ARE NOT ALONE

"I can’t give solutions to all of life’s problems, doubts, or fears. But I can listen to you, and together we will search for answers."

karibuni

Karibuni katika blog yetu ambayo itakuwa ikizungumzia kuhusu masuala ya uzazi hasa kwa wale wenye matatizo ya kuchelewa kupata watoto (infertility). Hapa tutajadili chanzo cha matatizo hayo na njia zinazoweza kutumika kuondoa tatizo hilo pamoja na kupeana ushauri na nasaha katika masuala mbalimbali yanayohusu uzazi. "KWA NEEMA YA MUNGU KILA MWANAMKE ATANYONYESHA"

Monday, 27 February 2012

Story Yangu -2

safari yangu ilianzia miezi michache baada ya kufunga ndoa, kusema kweli ile miezi sita ya mwanzo sikuwa na wasiwasi sana hasa kwa vile niliolewa mara tu baada ya kumaliza mitihani ya mwisho ya chuo, hata kabla ya graduation hivyo kulikuwa na kipindi cha kufanya mazoezi kwa vitendo (field) na muda wa kutafuta kazi, kwangu niliona sawa tu nikipata au nisipopata kwa wakati ule kwavile nilikuwa bado najipanga kimaisha.

baada ya miezi sita kupita ukizingatia kuwa sikuwahi kutumia njia yoyote ya uzazi katika maisha maisha yangu ndio sasa nikaanza kuwa na wasi wasi ingawa pia bado wakati huo sikuwa na ile presha saaana  ya kupata mtoto, basi katika kuongea na familia yangu kuhusu jambo hilo wakanipatia dawa za kiasili nikumie tukiamini kuwa zitasaidia, nilitumia kama miezi minne mfululizo bila mafanikio yoyote.

hapo sasa ndio hofu ikaningia, huyo mbio mpaka hospitali (naomba nihifadhi jina la hospitali hii ili kulinda heshima yao, inawezekana sikufanikiwa mimi ila wapo waliofanikiwa hapo hapo kwani matatizo hayalingani) nilikutana na daktari akaniandikia dawa na kurudi zangu nyumbani, baada kutumia dawa hizo tatizo jipya kijitokeza, nikaaza kubleed haikuwa nyingi sana ila ilikuwa ya muda mrefu nilibleed kwa zaidi ya miezi tisa mfululizo, ilikuwa ikiacha labda siku moja yapili inarudi tena, au napumzika asubuhi jioni tena, basi hayo yakawa ndio maisha yangu kwa takriban mwaka mzima. nilikosa raha jamani nikasema mimba sipati sasa hiki nini tena jamani. Ukiniuliza ni dawa gani ilinisaidia siijui maana nilikunywa kila kilicholetwa mbele yamgu, vidonge vya hospitali, majani hadi mizizi nahangaika kutafuta uzima wangu. nashukuru mungu nilipona mwanzoni mwa mwaka 2006.

katika hangaika yetu mwaka huohuo 2006 tulipata habari za kuanzishwa kwa kituo ama clinic ya kina mama katika hospitali ya Muhimbili. ilikuwa ikiitwa WELL WOMAN CLINIC, ilikuwa ni kitengo maalum cha kuwapima na kuwatibia kina mama tu, na huduma zao zilikuwa ni nzuri sana sijui ni kwanini waliacha kikafa kile kitengo. Basi nikafika hapo na kuhudumiwa vizuri sana. walinifanyia vipimo vyote hadi kansa ya kizazi, baada ya kuridhika na majibu ya awali nikapangiwa gyno ambaye alinitaka nifanye vipimo vya ziada viwili, nilipima  mirija na kukuta iko sawa, nikafanya ultra-sound ambayo ilionyesha kuwa nina PCOS. basi matibabu yakaanza, aliniandikia METFOMIN ( vidonge hivi hutumia na wagonjwa wa kisukari ndio dawa yao kubwa) ambayo nilitakiwa kunywa kwa miezi mitatu kama ikipita hiyo sijafanikiwa basi nirudi tena hospitali.

ANGALIZO: ingawa metfomin ni dawa za wagonjwa wa kisukari ila zinatumika sana kutibu PCOS ni moja kati ya dawa kuu zinazotegemewa kwani PCOs inahusiana na insulin resistance. 
kwa wale wenye PCOS mnaweza kutembelea mtandao huu ambao ni kama forum kwa watu wenye PCOS  tu, hapo unaweza uliza swali lolote ukapata majibu,  inaweza kuwasaidia  www.soulcysters.com

 xxxxxxxxxxxxxxx narudi sasa hivi...................................


1 comment:

  1. Infertility clinics are specifically for couples who encounter problems when it comes to conceiving a baby. The professionals in these clinics also work with couples who want to undergo some treatment for their fertility issues and also for individuals and same-sex couples who wish to have children of their own.

    Infertility Clinic

    ReplyDelete