YOU ARE NOT ALONE

"I can’t give solutions to all of life’s problems, doubts, or fears. But I can listen to you, and together we will search for answers."

karibuni

Karibuni katika blog yetu ambayo itakuwa ikizungumzia kuhusu masuala ya uzazi hasa kwa wale wenye matatizo ya kuchelewa kupata watoto (infertility). Hapa tutajadili chanzo cha matatizo hayo na njia zinazoweza kutumika kuondoa tatizo hilo pamoja na kupeana ushauri na nasaha katika masuala mbalimbali yanayohusu uzazi. "KWA NEEMA YA MUNGU KILA MWANAMKE ATANYONYESHA"
Showing posts with label TANGAZO. Show all posts
Showing posts with label TANGAZO. Show all posts

Friday, 21 March 2014

TUNARUDI HEWANI

Habari za siku nyingi wapendwa.

Kutokana na sababu mbali mbali za kifamilia na binafsi (ikiwemo shule), nilipumzika kuweka post kwa muda mrefu, hata hivyo ndani ya muda wote huo nimekuwa nikipokea emails mbali mbali kutoka kwa wasaka wenzangu zikiniomba niendelee kublogua. Katika siku tatu zilizopita email zimeongezeka na kuna ambazo zina ujumbe mzito sana kiasi ya kwamba ilinibidi nikae chini na kufikiria maamuzi yangu tena. Nimewaza na kujiuliza:-
- hivi ni lipi lengo la kuanzisha hii blog na sasa niwaache mkono wasaka wenzangu ambao wanahitaji mahali pakusemea shida zao na mahali pa kupumua wakati nayajua fika magumu na maumivu ya tatizo hili hasa unapokua mpweke?

Baada ya kupata majibu ya suali hilo nimeamua kurudi tena hewani kwa lengo lile lile la kusaidia, kupeana ushauri, kufarijiana, kupeana nguvu na moyo ili tuweze kupambana na hili tatizo letu, hivyo basi nawatangazia rasmi kuwa tutaanza kublogua kuanzia  Jumaatatu tarehe 24 March 2014.

Kwa kweli ushirikiano wenu unahitajika sana ili tuweze kufanikiwa na lengo letu litimie. nakaribisha mtu mwenye makala yoyote ambayo inahusiana na usaka, maswali, maoni,  ushauri, ujumbe, ushuhuda hasa kwa waliofanikiwa ili waweze kuhamashisa wengine, n.k. 
Nawashukuru sana kwa umoja na ushirikiano wenu.
Msaka mimi,
Chaby

Note: nakaribisha maoni pia kuhusu muonekano mzima wa blog nini tuongeze na nini tupunguze ili kuipendezesha.

Sunday, 6 May 2012

NIMERUDI

Habari wapendwa, samahani kwa kutokuwa nanyi kwa muda, nilizidiwa kidogo na majukumu ya kikazi, kifamilia na pia nilipatwa na msiba wa kaka yangu. Kwa muda wote wote huo mlikuwa mawazoni mwangu na nikaahidi nikipata nafasi tu nitaandika niwajulishe kuwa tuko pamoja.
Kwanza niwape mrejesho wa ile siri yetu, tulifanikiwa kuipata na kila mmoja wetu kati ya wasaka 10 (kama ulitusahau ingia hapa kikosi kamili) anaendelea na mapambano. Mimi binafsi nilishatumia mwezi uliopita na sasa nimerudia mara ya pili nasubiri matokeo... kujua zaidi kuhusu kitakachojiri usikose kusoma ile sehemu yetu pendwa "SAFARI YA WASAKA". Bila kusahau, maombi na dua zenu bado zinahitajika kwa saaana.

Tuesday, 28 February 2012

Kauli Mbiu

Wadau,
kuna mdau anony wa pili kuchangia kwenye STORY YANGU -1 alitoa maoni yake mwisho akasema atasapoti ili "kila mwanamke anyonyeshe"   mnaonaje hayo maneno niliyopigia mstari tuyaongezee maneno  kidogo na ikawa ndio kauli mbiu yetu? nipeni mawazo yenu

Saturday, 25 February 2012

just a moment please

Wapendwa,
naomba mnivumilie kidogo tu muda si mrefu nitamalizia story yangu. nimepokea malalamiko mengi kuhusu kutomalizia story, naomba tuelewe kuwa lengo hapa ni kumsaidia mwanamke kwa kila njia, naweza kuandika story kwa mistari mitatu tu na nikamaliza, sawa itasaidia lakini sio wote kwani nitasema tu ilikuwaje nilifanya nini na ikawa nini. wakati kuna mwanamke mwenzetu ambaye yupo kwenye hali ngumu kumtoa hapo alipo na kumwambia aamini matokeo yako ni ngumu, pia lengo ni kusaidiana kupata kizazi na pia kimawazo na nasaha hata kwa wale ambao hawawezi kupata tena watoto.

pia tukumbuke kuwa blog yetu inagusa hisia nzito za watu, watu walioumia na wengine hata kukata tamaa ya maisha hivyo inabidi kujipanga kwa kila tutakaloongea ili mdau alipokee vizuri na liwe la msaada kwake ni kama mfano wa mtu mwenye ulemavu wa macho ukakurupuka na kumuita kipofu ni lazima ataumia ila ukitumia hilo la kwanza atakuelewa, hivyo uchaguzi wa maneno au lugha safi pia unachangia kuchelewa huko.

jambo lingine ni kuwa hapa naongelea historia ya maisha ya ukweli na sio hadithi ya kutunga wala maigizo ambayo inashirikisha watu wengi, inabidi kuwa makini pia na maelezo kwani pamoja na kuwa wapo na wanatukwaza kwa shida zetu hizi lakini bado pia watu hao ni sehemu ya maisha yetu na jamii inayotuzunguka hivyo pamoja na yote tunahitaji kuwa na mahusiano mema nao.

naomba tushirikiane kwa wale wote wenye maoni, michango au ushuhuda mniandikie kupitia e-mail yangu sanraznassy@hotmail.com nami nitayaweka hadharani ili kila mwanamke afaidike. muda si mrefu nitatoa namba ya simu tuwasiliane.

kwa wale wanaohitaji kujua siri yangu pliz nitumieni email pia mniandikie na contact zenu tutawasiliana. sio siri kubwa ila napenda kuongea nanyi private ili kulinda heshima za watu mbali mbali akiwemo mwenza wangu.

tushirikiane, pamoja tutashinda.