YOU ARE NOT ALONE

"I can’t give solutions to all of life’s problems, doubts, or fears. But I can listen to you, and together we will search for answers."

karibuni

Karibuni katika blog yetu ambayo itakuwa ikizungumzia kuhusu masuala ya uzazi hasa kwa wale wenye matatizo ya kuchelewa kupata watoto (infertility). Hapa tutajadili chanzo cha matatizo hayo na njia zinazoweza kutumika kuondoa tatizo hilo pamoja na kupeana ushauri na nasaha katika masuala mbalimbali yanayohusu uzazi. "KWA NEEMA YA MUNGU KILA MWANAMKE ATANYONYESHA"

Friday 11 May 2012

JIACHIE: Unapokutana na vitu vya watoto madukani unajisikiaje?

katika kitu ambacho huwezi kukiepuka ni kuona vitu vya watoto, hasa ukiwa ni mtu unaependa kutembea sana madukani. hebu mdau leo funguka useme  unavyojisikia pale unapokutana navyo....

pangine familia haikuelewi, wakwe ndio usiseme, huenda hata na mume nae hakusomi vizuri. kwanini ufe na tai shingoni!!! jiachie shosti hapa ndio penyewe, mwanamke na uzazi ipo kwa ajili yako.

blue baby bootiesblue baby crib baby bottlepink diaperbaby comb and brush

basi niwaambie ya kwangu; msinicheke lakini.. au nijicheke mwenyewe? hahahaahha!!
kuna siku mwenzenu nilienda mlimani city wakati bado mpya mpya, na mimi wakati huo ndio nasaka kwa kwenda mbele, nikajidai kuingia game na mimi nikashangae lol!!! basi nikatembea tembea nikakutana na ile section ya watoto, na wanavyojua kupanga vitu vizuri basi, nikajisogeza duh nikaona vitu vizuriiiii lakini ndio sina uwezo wa kuvinunua. Jamani mwenzenu niliganda pale nilipokuwa kama nimewekwa super glue, miguu hata kunyanyua siwezi, nikahisi kama kitu kimenikaba rohoni  na machozi yanataka kunitoka, nikamuona muhudumu anatembea kuelekea nilipo mimi basi ikabidi nijikaze nikafanya kama natoa kitu machoni kumbe nafuta machozi huyoooo nikaishia zangu na mlimani city hapakukalika tena

5 comments:

  1. hahaaa pole sana.. I love ur story....Mie huwa nanunua kabisa naweka kabatini muda ukipita au nikisikia rafiki yangu kajifungua basi nabeba naenda kumpa zawadi..Ila nia taulo hilo la mtoto wa kiume maana lina u blue kidogo nilinunua mwaka 2008 nimelitunza hadi leo, pia nina magauni gauni mawili yana zaidi ya mwaka..kwa wakristo wanasema....kama kweli umeamini kuna uponyaji wa muujiza basi chukua hatua ya kiimani...means ninanunua nguo kwa maana ninaamini nitanyonyesha..kununua nguo ni hatua ya imani kwangu.

    ReplyDelete
  2. zamani nilikua na mtindo wa kununa na kuweka, nikidhani kuwa ipo siku nitapata wangu na atavitumia, lakini kadiri kupata ujauzito ulivyozidi kuwa mgumu, nilivigawa, vilinipa kumbukumbu ya majonzi nikiviona! Kwa sasa hivi nina matumaini, nitasimama, na kuangalia bidhaa, au pia hupita bila roho kuniuma, najua ipo siku na mimi nitakuwa mteja hapo, sijui kwa nini lakini nina imani sana.

    desparateme

    ReplyDelete
    Replies
    1. Yaani Dada Desperate Amini kuwa umeshapata...mwaka huu lazima kieleweke..

      Delete
    2. AMINA Shelyc! mdomo wako uwe wa kheri! na wote tunaohangaika humu ndani pia kitaeleweka! hizi hodi zote tunazopiga lazima milango ifunguliwe tuu.

      Delete
  3. jaman mie mwenzenu nina mwaka wa 5 sasa ila sijakata tamaa pia,zamani ndo ilikua inanipa shida nikikutana na nguo za watoto roho inaumaaaa weee,ila sasa hivi hata siumii tena kama mwanzo na mtoto bado natafuta

    ReplyDelete