YOU ARE NOT ALONE

"I can’t give solutions to all of life’s problems, doubts, or fears. But I can listen to you, and together we will search for answers."

karibuni

Karibuni katika blog yetu ambayo itakuwa ikizungumzia kuhusu masuala ya uzazi hasa kwa wale wenye matatizo ya kuchelewa kupata watoto (infertility). Hapa tutajadili chanzo cha matatizo hayo na njia zinazoweza kutumika kuondoa tatizo hilo pamoja na kupeana ushauri na nasaha katika masuala mbalimbali yanayohusu uzazi. "KWA NEEMA YA MUNGU KILA MWANAMKE ATANYONYESHA"

Sunday 6 May 2012

NIMERUDI

Habari wapendwa, samahani kwa kutokuwa nanyi kwa muda, nilizidiwa kidogo na majukumu ya kikazi, kifamilia na pia nilipatwa na msiba wa kaka yangu. Kwa muda wote wote huo mlikuwa mawazoni mwangu na nikaahidi nikipata nafasi tu nitaandika niwajulishe kuwa tuko pamoja.
Kwanza niwape mrejesho wa ile siri yetu, tulifanikiwa kuipata na kila mmoja wetu kati ya wasaka 10 (kama ulitusahau ingia hapa kikosi kamili) anaendelea na mapambano. Mimi binafsi nilishatumia mwezi uliopita na sasa nimerudia mara ya pili nasubiri matokeo... kujua zaidi kuhusu kitakachojiri usikose kusoma ile sehemu yetu pendwa "SAFARI YA WASAKA". Bila kusahau, maombi na dua zenu bado zinahitajika kwa saaana.

3 comments:

  1. karibu tena na pole kwa msiba na majukumu yalikubana,...tuko pamoja one luv.
    severina.

    ReplyDelete
  2. Pole sana dada..Mwenzenu naingia kwenye blog kila siku kuona yaliyojiri...Naamini very soon kutakuwa na breaking newsss nzuri...Tupo pamoja

    ReplyDelete
  3. nashukuru sana kwa kunipa faraja na kuwa na mimi. hata mimi ninaamini very soon tutapata good news

    ReplyDelete