YOU ARE NOT ALONE

"I can’t give solutions to all of life’s problems, doubts, or fears. But I can listen to you, and together we will search for answers."

karibuni

Karibuni katika blog yetu ambayo itakuwa ikizungumzia kuhusu masuala ya uzazi hasa kwa wale wenye matatizo ya kuchelewa kupata watoto (infertility). Hapa tutajadili chanzo cha matatizo hayo na njia zinazoweza kutumika kuondoa tatizo hilo pamoja na kupeana ushauri na nasaha katika masuala mbalimbali yanayohusu uzazi. "KWA NEEMA YA MUNGU KILA MWANAMKE ATANYONYESHA"

Friday 25 May 2012

Safari ya Wasaka: GOOD NEWS

Wadau nina furaha kubwa sana kuwapa taarifa kuwa msaka mmoja kati yetu amepata POSITIVE PREGNANCY TEST RESULT. Habari hizi tayari zimeshathibishwa na daktari.
Kujua ni msaka yupi huyo na safari yake ilikuwaje, usicheze mbali na hapa nitakuletea profile yake, tusubiri kidogo baby wetu atulie tumboni si mwajua tena tulivyosaka!!!  Kwa niaba ya wasaka team, nachukua nafasi hii kukupongeza mpendwa wetu, mungu akusaidie na akukuzie mtoto wako, na akupe safari nyepesi hadi kujifungua salama bila ya matatizo. KWA NEEMA YA MUNGU KILA MWANAMKE ATANYONYESHA..... SAFARI BADO YAENDELEA....

2 comments:

  1. Mpe hongera zangu nyingi sanaaaaa...nilikuwa safarini maporini no internet......Hongera sanaaaa

    ReplyDelete
  2. Jamani Mungu amzidishie amuwekee mwanawe! Tukaze buti kuomba na kujiamini hakuna kukata tamaaaaaaaaaa.

    ReplyDelete