YOU ARE NOT ALONE

"I can’t give solutions to all of life’s problems, doubts, or fears. But I can listen to you, and together we will search for answers."

karibuni

Karibuni katika blog yetu ambayo itakuwa ikizungumzia kuhusu masuala ya uzazi hasa kwa wale wenye matatizo ya kuchelewa kupata watoto (infertility). Hapa tutajadili chanzo cha matatizo hayo na njia zinazoweza kutumika kuondoa tatizo hilo pamoja na kupeana ushauri na nasaha katika masuala mbalimbali yanayohusu uzazi. "KWA NEEMA YA MUNGU KILA MWANAMKE ATANYONYESHA"

Friday 11 May 2012

KUELEKEA SIKU YA WAMAMA DUNIANI*** SPECIAL DEDICATION KWA WASAKA WOTE

Katika kuelekea siku ya wamama duniani, naomba nitoe wimbo huu kama maalum kwa wasaka wote. wimbo huu unaonesha ni kiasi gani kila mwanamke anahitaji kuwa mama na kuwa na familia, hii ni kutokana na heshima tunazopewa na mama zetu, na faraja tunazozipata kwa kuwa nao.  Hivyo nasi tunatamani kuwa kama wao. Tunawasukuru mama zetu kwa kutuzaa, kutulea vizuri na kwa mapenzi yote mnayoendelea kutuonyesha, tunawaomba wamama na wanawake wote mtupe sapoti  katika safari yetu hii kwa kila njia inayowezekana ili sote mwakani tuwe tunaitwa Mama. YES..... i would die for that.

SHUKRANI MAALUM KWA MAMA YANGU MZAZI, NAJUA UNANIPENDA NA KUNISAIDIA KWA KILA HALI, ILA UKWELI SIKUJUA NI KIASI GANI ULIKUWA UKIUMIA KWA KUCHELEWA KWANGU KUPATA MTOTO HADI SIKU NILIYOJIFUNGUA NA KUNIAMBIA KUWA ULIWEKA NADHIRI KIKIZAA UTASOMA MAULID  NILIPATWA NA MSHANGAO NA SIKUJUA NIKUAMBIE NINI. AHSANTE SANA MAMA, YOU ARE THE BEST, LOVE YOU SOOOOO MUCH.

No comments:

Post a Comment