YOU ARE NOT ALONE

"I can’t give solutions to all of life’s problems, doubts, or fears. But I can listen to you, and together we will search for answers."

karibuni

Karibuni katika blog yetu ambayo itakuwa ikizungumzia kuhusu masuala ya uzazi hasa kwa wale wenye matatizo ya kuchelewa kupata watoto (infertility). Hapa tutajadili chanzo cha matatizo hayo na njia zinazoweza kutumika kuondoa tatizo hilo pamoja na kupeana ushauri na nasaha katika masuala mbalimbali yanayohusu uzazi. "KWA NEEMA YA MUNGU KILA MWANAMKE ATANYONYESHA"

Thursday 2 February 2012

Story Yangu - 1


Kawaida binaadamu tumeumbwa na tamaa, iwe ni ya afya, mali, watoto, vyeo na mengineyo na kila mtu kwenye ulimwengu ana kitu ambacho anakitamani. lakini wengi kati yetu hasa wanawake huwa na tamaa ya kupata mwenza  wako, mkaishi kama mke na mume na mpate watoto...... na tamaa hii iko wazi na wala haijifichi miongoni mwa wengi.

kati ya hao wanaotamani mimi ni mmoja wapo, tamaa yangu ilianza mwaka 2004 baada ya kufunga ndoa, nilianza kuhesabu.... siku zikapita........miezi ikakata! na miaka ikapotea.!!!! lakini sikubarikiwa. what is wrong????  nilianza kujiuliza. Kufikia hapo tamaa  iligeuka ikawa ni mawazo,  hasira na kila unachokijua ambacho mtu humtokea pindi unapokosa kitu fulani unachokihitaji  zaidi, hasa ikiwa jamii inayokuzunguka haikuelewi na inategemea utende mambo ambayo yapo nje ya uwezo wako na miujiza ambayo hujabarikiwa. Naamini kwa ambaye amewahi pitia njia hii au bado yupo kwenye njia hii ananielewa zaidi.

Kama mjuavyo, msaka hachoki na akichoka basi keshapata! basi nami huyooooo kiguu na njia ........ mara kusi mara kaskazi nikisaka nisichojaaliwa.

lol hebu acha nipumue kwanza maana hii safari ni ndefu .....................tutakutana tena

12 comments:

  1. kwanza nakupa hongera sana kwa kufungua blog kama hii. Kwa kweli utawapa wanawake wengi moyo kwani kweli kama ulivyosema wanawake wengi limekuwa tatizo kama lako. Hawajui la kufanya bali ni kukata tamaa na msongo wa mawazo. Hongera sana. Nasubiri umalizie story yako.

    ReplyDelete
  2. nasukuru sana kwa kunipa moyo, wewe ndio wa kwanza umenitia nguvu na kunifanya niamini kuwa ninachokifanya ni sahihi. tuungane kumsaidia mwanamke pamoja tutashinda

    ReplyDelete
  3. Hongera mama kwa kuanzisha blog hii, itawagusa wengi hata wale wenye watoto, napenda niwatie moyo wanawake wenzangu, kwamba, kuzaa sio lazima ila ni majaaliwa ya Mwenyezi Mungu. Hata ukiwa na watoto, usijisifu na kujiona wewe umekamilika kuliko yule anayetafuta mtoto, unatakiwa kushukuru na kuwaombea wanawake wengine na ndipo mibaraka itajaa nyumbani mwako wewe na familia kwa ujumla. Nitasupport blog yako kwa michango na ushauri ili kila mwanamke anyonyeshe. ubarikiwe sana.

    ReplyDelete
  4. Msaka huwezi kuamini nilipoona hii blog cha kwanza kusema "Hasante Mungu" nina uhakika sasa nitapata ufumbuzi japo wa mawazo. Nami ni muhanga wa hilo nimeolewa nimedumu kwenye ndoa kwa miaka minne bila kufanikiwa mtoto, mume na ndugu zake wakashindwa kunivumilia, hapa ninapokwambia nimeachwa talaka tatu sababu ya kutokuzaa!! Mungu hamtupi mja wake nimepata mchumba mwengine ana moto na kiherehere anataka tufunge ndoa lakini naogopa nisije nikaadhirika tena. Mpendwa wangu niambie ulienda wapi ukafanikiwa! kuhusu hospital sina tatizo nimemaliza ma-Gyno wote hapa mjini, wanachoniambia labda nawazia sana ambayo nayo inachangia kutokupata mtoto. HIzo dawa za mabibi wa kihaya ndiyo husiseme hakuna dawa nisiyokunywa. Sasa naambiwa nina Ruhani akaombewe. Namimi naamini si tatizo la hospital. Je nifanyeje?

    ReplyDelete
  5. Ahsante kwa kutufungulia blog ambayo naamini itatupunguzia mawazo juu ya kutopata mtoto. Nami ni mhanga wa hilo jambo na nimemaliza ma-gyno wote lakin naambiwa hakuna tatizo kila k2 kipo sawa. Sasa hebu malizia hiyo story yako ili tujue ulifanyaje hadi ukafanikiwa mwenzetu.

    ReplyDelete
  6. dada Mungu akubariki kwa hii blog yako,nimepitia story yako though hujaimalizia bt nilipoisoma nahisi km unanizungumzia mimi,nipo ndoani almost5 yrs nw,cna mtoto,nimehangaika cna vipimo havioni tatizo,kila kitu normal,nimebaki kusubiri hatma yangu tu,ngoja nisubiri mwisho wa story yako mayb ntapata suluhu.
    Thanx,Mungu akuzidishie kwa kufikiria maisha ya watu km sisi.

    ReplyDelete
  7. Hi shamim

    Asante sana kwa blog hii itasaidia sana wanawake wengi.Ila ni kweli hayo matatizo yapo coz hata mie ninalo ila nadhan kwa ngu tofaui coz nina mtoto 1 wa kike na mwezi wa nane anatimiza miaka 6,ila uwezi amini sijawahi shika mimba tena na nilikuwa situmii uzazi wa mpango coz mume wangu alikuwa yupo kikazi mkoani mie nipo hapa Dar coz ya kazi.So toka hapo mpaka leo sijapata hata ya kusingizia nikaanza kwenda hosp kwa specialist nikapewa clomiphene na enat za vitamin so hizo enat unatumia mwezi mzima ila hizo clomiphene unaanza umia baada ya kumaliza period then ndio doctor anakupangia kukutana na mzee ili ushike mimba so nimetumia mpka nimechoka nilianza kwenda hosp mwaka jana mwezi wa nane coz may be nina tatizo nikapiga ultra sound sina tatizo so kila nikienda doctor ananipa dawa hizo hizo nami nimechoka kumeza nadhani hapa nitapata ufumbuzi wa ushauri na idea zingine ili nijue wai kwa kuanzia tena.

    Mungu akubari sana

    Mama Husna.

    ReplyDelete
  8. blog nzuri sana ...mi naomba katika kuyaongea haya tusisahau kwamba kuna wanawake wasio na tatizo ila ni waume zao na kutokana na culture yetu unakuta ni mwanamke tu ndo anahangaika kwa docta,madawa ya asili etc bila ya mwanaume naye kupimwa au kutumia hizo dawa za asili..naomba ktk kuelimisha huku usiache kufungua watu macho kwamba tatizo sio always mwanamke....gluck na blog

    ReplyDelete
  9. Hongera sana kwa kufungua blog ya namna hii,Mimi pia ni victim wa hili janga.Nipo kwenye ndoa mwaka wa nne nimehangaika kila njia.Tatizo langu ni hedhi,yaani napata mara moja au mbili kwa mwaka nilipoenda hospital waliniambia nina PCOS,Wakasema inawezekana kutibu hilo tatizo lakini itachukua muda mrefu sana,So walichonishauri nifanye IVF Yaani kupandikizwa mbegu na yai,Ni gharama sana kma ningelipa mwenyewe uzuri ni kwamba naishi ulaya kwa hiyo Serikali ikaamua kunisaidia.Nimejaribu mara ya kwanza hola ya pili hola na hivi nasubiri ya tatu.Roho inaniuma sana rafiki zangu wote wana watoto.Kila nikikutana nao wananiuliza nitazaa lini?.Sina cha kujibu nabaki kutokwa na machozi.Ila kamwe siwezi kata tamaa najua ipo siku Mungu atajibu maombi yangu.Nataka kujaribu njia za kienyeji kwa wale ambao mko TZ tafadhali kama kuna mtu mnamfahamu anasaidia naomba mniambe.

    ReplyDelete
  10. kwa kweli,Mungu akubariki sana katika safari hii ya kuanzisha blog na kupata mahala ambapo wanawake wenye matatizo kama haya watachangia..nitawapa ujumbe na wengine waje humu wa aina hii ,tukawa na umoja ili tuwe na nguvu.inauma sana..unapotegemea kuwa na mtoto halafu hupati...nami nilipita huko huko..na nimewahi kufikiri jinsi ya kuungana na watu KUWEZA KUSAIDIA WALE AMBAO WAKO KATIKA SHIDA HIYO.NILIBAHATIKA KUPATA MUME MWENYE UPENDO..HAKUNISALITI..NA ALINIPA MOYO AKANIAMBIA..ZAMU YANGU INAKUJA..SASA NINA MTOTO..NA WALA ,ALIKUJA TU WHEN WE DIDNT EXPECT..KAMA MUUJIZA..WATOTO NI BARAKA TOKA KWA MUNGU..NA AMBAYE HAJAPATA ..ZAMU YAKE YAJA..MIMI NI MKE WA DAKTARI..KWA UPANDE FULANI HII ILISAIDIA..TUTAWASILIANA ZAIDI..WANAWAKE OYE!! TUSIKATE TAMAA..WE ARE BEAUTIFUL,WITH OR WITHOUT CHILDREN..NAWAPENDA SANA.

    ReplyDelete
  11. nimeipenda hii blog mami...wewe ni mwanamke mwenye akili sana...najua hapo mbele unaweza kuja kua waziri wa wanawake...keep up the good job dear..

    ReplyDelete
  12. Hata mie nilifurahi kuona umeanzisha blog ya aina hii, lakini nilikua na matumaini makubwa sana kwamba nikiingia nitakuta tayari formulas, fanya hivi, jaribu hivi kama mimi, na kadhalika, badala yake nimekuta story, ambayo imeishia katikati, kana kwamba ni mtego kwa mtu kufuatilia blog! elewa mwanamke anayetafuta mtoto, hataki mafumbo, anataka kupewa mawaidha papo hapo! sio kama kwa mganga, njoo kesho, njoo keshokutwa! naona iwapo umeamua kuwapa watu historia yako na jinsi ulivyofanikiwa, basi fanya. asante.

    ReplyDelete