YOU ARE NOT ALONE

"I can’t give solutions to all of life’s problems, doubts, or fears. But I can listen to you, and together we will search for answers."

karibuni

Karibuni katika blog yetu ambayo itakuwa ikizungumzia kuhusu masuala ya uzazi hasa kwa wale wenye matatizo ya kuchelewa kupata watoto (infertility). Hapa tutajadili chanzo cha matatizo hayo na njia zinazoweza kutumika kuondoa tatizo hilo pamoja na kupeana ushauri na nasaha katika masuala mbalimbali yanayohusu uzazi. "KWA NEEMA YA MUNGU KILA MWANAMKE ATANYONYESHA"

Tuesday 28 February 2012

Story Yangu -3

nilitumia metformin kwa miezi sita bila mafanikio na nikaanza kukata tamaa, hasa baada ya mume wangu kupata nafasi ya masomo nje ya nchi. hapo sasa niliona mimi kuzaa ndio historia nitaishia kuitaja tu na hata zile dawa nikaacha kutumia.

kwa bahati nzuri safari yake haikuwa kikwazo sana kwani alikuwa akirudi nyumbani mara kwa mara, aliondoka mwishoni september na december akarudi hivyo haikuniathiri sana. Hapo sasa nilirudi hospitali na nikapewa dawa za aina 2, kuna ambazo unakunywa kila siku na zingine ndio zile unakunywa MP tu ikiisha kuhesabu siku. nilikuwa nakunywa kila akiwa anarudi tanzania, nazo pia sikufanikiwa, nikaambiwa sasa inabidi nifanyiwe opareshen kuangalia kama kuna ukungu utolewe!!!! nini!!! opareshen kuangalia kama kuna ukungu!!!? kama huo ukungu upo sawa itakuwa nimepata tiba, kama haupo je???!!!! mmh ilikuwa ngumu kuamua kwa kweli kupasuliwa kwa majaribio... hapana moyo uligoma, sikurudi kupasuliwa. baada ya hali hiyo mwezi december 2007 nikaamua kusafiri nami nikiwa na tamaa walau nitapata matibabu zaidi.

nilienda hospitali ya kwanza, nilieleza historia yangu yote na kufanyiwa vipimo. daktari akasema kuwa haoni tatizo lolote kila kitu kipo sawa. hakunipa hata  dawa ya maumivu, ila alinielekeza niende hospitali nyengine kwa daktari bingwa zaidi. nakumbuka huyu mama aliniambia maneno ambayo yalinitia nguvu sana, naomba ninukuu baadhi ya maneno aliyoniambia kwa faida ya wanawake wenzangu.

alisema hivi " najua unaumia kwa sasa, lakini jaribu kuishi hizi siku zako kwa raha zote kwani utakapoanza kupata watoto utaukumbuka huu muda na kutamani urudi tena" (ni kweli unaitamani ile free time baada ya majukumu kuongezeka, ingawa faraja ya kuwa mama inakupa nguvu ya kupambana na maisha) alisema yeye alipata mtoto wa kwanza akiwa na miaka 38 

basi, nikaenda hospitali nyengine ambako ni kwa gyno bingwa, naye pia alinipima na kuniambiwa kuwa haoni tatizo lolote kila kitu kipo sawa sawa. akanipima na matiti akasema matiti yangu yanaonesha ninao uwezo wa kuzaa. nako sikupewa dawa, sasa nikawa najiuliza ile PCOS imeenda wapi? au ndio zile dawa zilinisaidia? lakini mbona wanasema PCOS huwa haiponi? sijui na mpaka sasa bado sijapata hili jawabu. nikarudi zangu Tz nikiwa na maswali mengi kichwani ingawa nilikuwa na tamaa baada ya yale majibu ya madaktari. 

hapo sasa niliamua kujitibia mwenyewe, nilishachoka na safari za hospitali kila siku. nilikuwa kama kichaa nusu mwendawazimu, nalala na mtandao naamka na mtandao, nilitafuta kila kitu kinachohusiana na uzazi,  matatizo, chanzo chake ma matibabu, ingelikuwa kutibia watu sio lazima ukasome vyuoni basi mimi ningebadilisha utaalamu na kuwa gyno. ilifika wakati hata nikiwa njiani niko na makaratasi yangu nasoma.

niliendelea kutafuta suluhisho  hadi mwishoni mwa 2008 ndio nikakutana na hiyo siri yetu. nashukuru mungu mwezi huo huo mambo yakawa mazuri na August 2009 nikajifungua mtoto wa kiume.

mwaka 2010 nilipata ujauzito mwingine na ilikuja tu yenyewe bila kutegemea lakini niilipata bahati mbaya ikiwa na miezi miwili. nikaamua kupumzika. sasa natamani mtoto wa pili ambapo nimejaribu kawaida mpaka sasa bila mafanikio, na nataka kuirudia siri yetu..............

nimejifikiria mimi na pia kuwafikiria wenzangu ambao nao ni wahanga, ndio nikaona bora kuanzisha blog ili tupate sehemu yetu ya kupeana mawazo, ushauri na kupeana moyo. kwa wale wote wasaka wenzangu twende pamoja.....................tutaiona njia kwa uwezo wa mungu.

na kwa nyote mliobarikiwa tunawahitaji kwa msaada wa mawazo na ushirikiano ili tupate nguvu ya kupambana na majaribu haya.

kwa anaetaka kujua hiyo siri tuwasiliane kwa email yangu sanraznassy@hotmail.com muda wowote. 

1 comment:

  1. Nimekuwa so touched na story yako ntakutafuta kwenye email uliyotoa kwani nna matatizo kama hayo uliyokuwa nayo

    ReplyDelete