YOU ARE NOT ALONE

"I can’t give solutions to all of life’s problems, doubts, or fears. But I can listen to you, and together we will search for answers."

karibuni

Karibuni katika blog yetu ambayo itakuwa ikizungumzia kuhusu masuala ya uzazi hasa kwa wale wenye matatizo ya kuchelewa kupata watoto (infertility). Hapa tutajadili chanzo cha matatizo hayo na njia zinazoweza kutumika kuondoa tatizo hilo pamoja na kupeana ushauri na nasaha katika masuala mbalimbali yanayohusu uzazi. "KWA NEEMA YA MUNGU KILA MWANAMKE ATANYONYESHA"

Tuesday 28 February 2012

Kauli Mbiu

Wadau,
kuna mdau anony wa pili kuchangia kwenye STORY YANGU -1 alitoa maoni yake mwisho akasema atasapoti ili "kila mwanamke anyonyeshe"   mnaonaje hayo maneno niliyopigia mstari tuyaongezee maneno  kidogo na ikawa ndio kauli mbiu yetu? nipeni mawazo yenu

2 comments:

  1. Bi Msaka,

    Nimefarijika sana wewe kuona neno la " kila mwanamke anyonyeshe" limekuwa neno zuri kwako. Neno hilo huwa nalitumia sana ninapowaombea wanawake wanaotafuta watoto, na wengi wao kwa kweli wamefanikiwa. Ushauri juu ya neno hili, tulipe nguvu za Ki-Mungu zaidi ili lisiwe karaha kwa wale wasiokuwa na watoto na hasa wale wanaotafuta watoto kwa muda mrefu.

    Labda nitoe mfano kauli mbiu hii iweje bila kumkwaza Muumba na viumbe wake,Kwa mfano, "Kwa mapenzi yake Mola, kila Mwanamke atanyonyesha" au "Mwenyezi anapenda kila mwanamke anyonyeshe" au Mungu ni mwema, wanawake wote wanyonyeshe!.

    Nasema hivi kwa sababu mwisho wa furaha yetu yote hii ya kuwa na mtoto ni Mungu Muumba ambaye hushiriki kwa 100%. Tumuenzi Muumba kwa hili kwani hata tusipokuwa na watoto yeye ndio kimbilio letu. Tukiacha neno "kila mwanamke anyonyeshe" nina wasiwasi litatumika vibaya na sisi wanawake hasa katika kuwakebehi wanaotafuta watoto (kwani wapo wanawake wa aina hiyo ambao huwasema vibaya wanawake ambao wanatafuta watoto). Nitakutumia email yangu kwa mawasiliano zaidi. Mungu azidi kutubariki wanawake wote ulimwenguni.

    Nawapenda,

    Mama Smile!

    ReplyDelete
  2. Kweli Mungu azidi kukubarik na kukupa hekima,mana kila nikifungua humu nakutana na maneno ya faraja kiac kwamba najihic tatizo langu linafikia mwisho wake!kweli huo msemo utafaa iwapo tutauongezea kama mdau hapo alivyosema nafikiri itafaa sana kama utasomeka kwa Neema ya Mungu kila mwanamke anyonyeshe'ni mawazo yangu tu kama yatafaa..thanx'

    ReplyDelete